Lugendo : Shirika NDSCI linaomba watoto waachishwe migodi, wazazi wasaidie kurudisha shuleni

Published from Blogger Prime Android App

Siku chache kabla ya kufunguliwa kwa masomo, watoto wengi kutoka Lugendo na Ishungu wanaendelea kukimbilia kwenye mgodi wa Lomera kwa ajili ya kutafuta fedha. Hali hii imewafanya wengine kusahau masomo na kuacha kusikiliza ushauri wa wazazi.

Radio Club Lugendo kwa kushirikiana na NDSCI wametoa wito kwa viongozi wa eneo hilo kuhakikisha watoto wote wanaopatikana migodini wanarudishwa nyumbani na kuandaliwa kwa shule.

Mwenyekiti wa Shirika la kiraiya NDSCI ya Lugendo, Raha Lukas, alisema:

"Watoto ni wanafunzi, siyo wafanyakazi wa migodini. Tunawaomba viongozi wachukue hatua madhubuti kuwalinda ili wasipoteze ndoto zao."

Wito kwa wazazi na watumiaji wa watoto

Mashirika haya pia yanawakumbusha wazazi kuhakikisha wanawaongoza watoto wao na kuwasihi kutoacha shule kwa tamaa ya fedha ndogo zinazopatikana migodini. Wazazi wanahimizwa kuwa walinzi wa kwanza wa elimu ya watoto wao.

Vilevile, watu wazima wanaotumia watoto kama nguvu kazi migodini au kwenye mitumbwi wanaombwa kuacha mara moja tabia hiyo, kwani ni kosa kisheria na ni hatari kwa maisha ya watoto.

Na kwa hitimisho, jamii yote ya Lugendo na Ishungu inahimizwa kushirikiana ili kulinda haki za watoto. Elimu ndiyo njia ya kuwafungulia mustakabali mwema, siyo migodi.

✍️ Tarifa hiyi imetolewa na Shirika NDSCI Lugendo, ikiandikwa na JEUNESSE & DÉVELOPPEMENT_RDC

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

Sud-Kivu : Le Médecin Chef de Zone de Miti-Murhesa dénonce une atteinte grave à la dignité des malades à l’Hôpital de Lwiro

Sud Kivu: cette déclaration du mouvement RSJDC relative à l'exploitation illicite de l'or au Sud Kivu

Sud-Kivu: la NDSCI Lugendo plaide pour la suppression des frais de participation au TENASOSP et EXETAT dans la partie Est de la RDC